Type Here to Get Search Results !

Yacouba Songne ndo hivyo Tena


 Yacouba Songne jana alicheza kwa takribani dakika 15 kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM

Kuingia kwake pamoja na kiungo Mudathir Yahya waliongeza kasi ya mashambulizi na hatimaye Yanga kufunga bao dakika ya 95 kupitia kwa Dickson Ambundo

Dakika 15 zilitosha kuwakumbusha Wananchi yule Yacouba wa mwanzoni mwa msimu uliopita

Yacouba huenda akapata dakika nyingi zaidi za kucheza kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Singida BS

Yacouba na Lazarus Kambole wamepewa nafasi katika michuano ya kombe la Mapinduzi benchi la ufundi likiwafanyia tathmini kuona utayari wao baada ya kuwa nje kwa muda mrefu wakiwa ni majeruhi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.