Type Here to Get Search Results !

Tetesi za usajili ligi kuu tz bara

 

Mshambuliaji wa Dalian Pro ya China, Cesar Manzoki raia wa Afrika ya Kati, anatajwa kuwasili Tanzania wiki hii kwaajili ya majadiliano na viongozi wa Simba kuona uwezekano wa kumsajili nyota huyo mwenye asili ya DR Congo.

Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa Kiungo wa zamani wa Vilabu vya Al-Hilal Club, JS Saoura na Moro United ya Morogoro, Thomas Ulimwengu kutoka Tp Mazembe ya DR Congo.

Kocha Mkuu wa muda wa Klabu ya Simba SC, Juma Mgunda ametajwa kutokuwa tayari kuwa Kocha msaidizi pale Simba SC na anataka kuondoka baada ya mchezo wa mwisho dhidi ya KVZ kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

KLABU ya Azam FC imekamilisha Usajili wa Golikipa wa kimataifa wa Ghana, Abdulai Iddrisu mwenye umri wa 25 kutoka Bechem United ya kwao Ghana.

Aliyekuwa Golikipa wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Hussein Abel amejiunga na klabu ya KMC FC ya Dar es Salaam.

Beki wa kushoto wa Geita Gold FC ya Geita, Yahaya Mbegu ameomba kuondoka katika Klabu hiyo endapo hatotimiziwa makubaliano ya mkataba wake.

Kiungo wa klabu ya Singida Big Stars FC ya Singida, Frank Zacharia amejiunga na KMC FC ya Dar es Salaam kwa mkopo wa nusu msimu (miezi 6)

Vilabu vya Dodoma Jiji na Namungo FC vinaiwinda saini ya beki wa pembeni wa Klabu ya Mbeya City ya Mbeya, Keneth Kunambi.

Klabu ya Ruvu Shooting FC imetangaza kukamilisha usajili wa Kiungo Mohamed Issa Banka kutoka Namungo FC.

Tetesi zinaeleza kuwa uongozi wa Yanga leo unatarajia kuvunja mkataba wa Mshambuliaji wao raia wa DR Congo, Heritier Ebenezer Makambo na nafasi yake kujazwa na Kiungo Mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Yacouba Sogne aliyerejea kutoka majeruhi, huku Lazarous Kambole akisubiri kwanza.

KLABU ya Mtibwa Sugar imetangaza rasmi kuachana na winga wake raia wa DR Congo, Deo Kanda mwenye umri wa miaka 33.

Klabu ya Young Africans bado ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Vipers kwaajili ya kupata saini ya kiungo wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Uganda Bobosi Byaruhanga mwenye umri wa miaka 21.

Singida Big Stars hadi sasa imeachana na Peterson Da Cruz , Amissi Tambwe, Kelvin Sabato na Daud Mbweni, huku waliosajiliwa mpaka sasa ni Enock Atta Agyei, Ibrahim Ajibu na Nickson Kibabage.

Kelvin Kongwe Sabato na Daudi Mbweni tayari wamesaini kuitumikia Polisi Tanzania FC wakitokea Singida Big Stars FC ya Singida.

Pia Ahmada Hilika ametua Polisi Tanzania akitokea Mtibwa Sugar FC ya Morogoro.

Uongozi wa Klabu ya Young Africans, umesema kuwa hauna mpango wa kuwaacha David Bryson, Dickson Ambundo na Yusuph Athuman kwa mkopo kwenda Klabu yeyote.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Felix Kone anayekipiga kutoka AS Kigali ya Rwanda anafuatiliwa kwa ukaribu na viongozi wa Simba, huku taarifa zikidai Mshambuliaji huyo anaweza kujiunga na Klabu hiyo yenye makazi yake Mtaa wa Msimbazi pindi dili hilo likikamilika.

Mshambuliaji wa klabu ya Power Dynamos ya kwao Zambia, Kenedy Musonda mwenye umri wa miaka 27 yupo kwenye rada za Klabu ya Simba SC.

Mshambuliaji huyo ambaye msimu huu ameshafunga mabao 13 kwenye mechi 17, amekuwa akiwindwa na klabu ya Amazulu ya Afrika Kusini.

Yanga SC inadaiwa kuitaka saini winga wa RS Berkane, Chadrack Muzungu Lukombe raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 25 kuja kuchukua nafasi ya Tuisila Kisinda ambaye anatajwa kuondolewa kikosini hapo.

Klabu ya Simba inapambana kuipata saini wa Mshambuliaji raia wa Ghana, Kwame Opoku ambaye kwa sasa anacheza kwa Mkopo Najran ya Saudi Arabia akitokea USM Alger ya Algeria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.