Type Here to Get Search Results !

Hawa hapa wachezaji watatu wanao waniwa na Simba Dirisha dogo hili la usajili

 

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wamejipanga kutumia vyema dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa usiku wa leo kufanya maboresho muhimu ya kikosi

Ahmed amesema wataleta wachezaji wa daraja la juu ambao watashirikiana na hawa waliopo katika kutimiza malengo ya klabu ya Simba msimu huu

"Usajili wa dirisha dogo lazima ulete watu kweli, watu ambao watakuwa na mchango mkubwa kwenye timu. Kwa sababu kwenye dirisha dogo husajili wachezaji wengi, labda wawili..watatu..mmoja lakini jambo muhimu lazima wachezaji hao waje waongeze kitu kwa hawa walipo"

"Wachezaji wetu wamepambana kutufikisha hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa hivyo mchezaji atakayesajiliwa lazima awe na mchango mkubwa kwenye mechi hizo za hatua ya makundi. Kwa hiyo niwahakikishie Wanamsimbazi, lazima tulete watu," alitamba Ahmed

Simba inahusishwa na wachezaji kadhaa katika dirisha hili lakini Cesor Manzoki, Saido Ntibazonkiza na Luis Miquissone wametajwa zaidi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.