Type Here to Get Search Results !

Simba Yatoa Ufafanuzi Wapi Yalipo Mabasi yao Mpaka Kutumia Coaster za Kukodi

 


KITENDO cha timu ya Simba kutotumia magari yao kwenye safari zake za hapa na pale pamoja na kwenda nayo uwanjani kwenye mechi kimeanza kuwashangaza wengi huku wakiwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Mabasi ya klabu ya Simba hayajashikiliwa kama inavyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii bali yapo katika ukarabati

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Ahmed Ally alisema mabasi yao hayaonekani kwa sababu yako gereji na sio kama ambavyo watu wamekuwa wakizungumza kuhusu kushikiliwa kwa sababu za kukiuka mikataba

Ahmed amesema taarifa zaidi zinaweza kutolewa na viongozi wa juu wa klabu lakini taarifa rasmi aliyonayo ni kuwa mabasi hayo yako gereji

"Wenye mamlaka ya kuzungumzia hayo ni viongozi wa Simba na mimi niseme tu wazi kwa mashabiki wetu kwamba mabasi yapo gereji pale Vingunguti, na yatakapokamilika kufanyiwa ukarabati mtayaona," alisema Ahmed

Katika siku za karibuni Simba imeonekana kutumia usafiri wa mabasi madogo 'coaster' kupeleka wachezaji uwanjani kwenye mechi na hata mazoezini kule Mo Simba Arena, Bunju

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.