Type Here to Get Search Results !

Yanga wakubali yaishe Kwa Feisal

 

Yanga inajipanga kumuongezea mkataba kiungo wake mshambuliaji Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga msimu huu akifunga mabao matano na kutoa pasi mbili za mabao

Thamani ya Feisal inazidi kupanda ofa zikiendelea kumiminika Jangwani kwa ajili ya kuisaka saini yake

Pamoja na kuwa bado ana mkataba zaidi ya mwaka mmoja na Yanga, mazungumzo yameanza ili kumuongezea mkataba ambao utaboresha maslahi yake mara dufu

Matajiri wa Azam Fc wanatajwa kumuwinda Feisal wakiweka ofa nono na mshahara mkubwa ambao ni zaidi ya Tsh Milioni 10 kwa mwezi

Ofa nyingine inatajwa kutoka kwa RS Berkane ambao wamekuwa na mahusiano mazuri na Yanga hasa baada ya usajili wa Tuisila Kisinda ambaye alisajiliwa na timu huyo na baadae kumruhusu arudi Yanga

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesisitiza kuwa hawatamzuia Feisal kujiunga na timu nyingine kama watapokea ofa sahihi lakini wangependa kuona anatoka nje ya mipaka ya Afrika

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.