Type Here to Get Search Results !

Huu hapa Ujumbe Wa Saido Kwa Mashabiki wote was Simba

 

Baada ya kuanza kwa kishindo ndani ya Simba akifunga mabao matatu 'Hat trick' na kutoa pasi ya bao moja, Saido Ntibanzokiza amesema huu ni mwanzo tu

Katika mechi yake ya kwanza akiwa na uzi wa wa Simba, Saido alikuwa chachu ya ushindi wa mabao 7-1 dhisi ya Prisons kwenye Dimba la Mkapa

Nyota huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Burundi, amesema amefurahi kuanza vyema majukumu yake kwa kufunga na kuasisti, huku akiweka wazi huo ni mwanzo tu wa mengi aliyowaandalia Wanasimba

"Nimefurahi kuanza hivi, ni mwanzo mzuri ambao nimeufurahia sana na naamini kwa mwendo huu nitafanya mazuri zaidi huko mbele" alisema Saido

"Nimefurahia mchezo na naamini kadiri siku zinavyokwenda tutazidi kuzoeana zaidi na wachezaji wenzangu kiuchezaji na tutatengeneza timu imara ambayo itawapa furaha mashabiki wetu"

Mabao matatu aliyoyafunga katika mchezo huo yamemfanya afikishe mabao saba kwenye ligi, huku pia akifikisha pasi saba za mabao sambamba na Ayoub Lyanga wa Azam wote wakiwa nyuma ya Chama mwenye nazo 11

Saido ameelekea visiwani Zanzibar akiwa na kikosi cha Simba kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo leo watashuka uwanja wa Amaan kupepetana na Mlandege

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.