Type Here to Get Search Results !

Simba kuanzia ugenini DHIDI ya Horoya Fc

 

Februari 10 mechi za hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika zitaanza kupigwa ambapo Simba iliyopangwa kundi C, itaanzia kugenini dhidi ya Horoya AC ya Guinea

Mechi ya kwanza nyumbani ambayo itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa ni Februari 17 dhidi ya Raja Casablanca

Februari 24 Simba itakuwa Uganda kumenyana na Vipers Fc  kisha kurejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Vipers Fc ambao utapigwa Machi 07

Machi 17 2023 Simba itashuka tena uwanja wa Benjamin Mkapa kukamilisha mchezo wa mwisho nyumbani dhidi ya Horoya Ac

Simba itakamilisha hatua ya makundi Morocco kwa kuikabili Raja Casablanca katika mchezo utakaopigwa April 01

Malengo ya Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa ni kutinga nusu fainali lakini kabla ya kuifikiria nusu fainali lazima wakate tiketi ya kutinga robo fainali

Alama zote tisa katika mechi za nyumbani ni lazima, halafu angalau alama mbili ugenini zitatosha kuipeleka Simba robo fainali

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.