Type Here to Get Search Results !

Hii hapa Ratiba kamili ya kombe la Shirikisho

Hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika itaanza kutimua vumbi Februari 12 2023, Yanga ikianzia ugenini nchini Tunisia dhidi ya US Monastir

Kwa mara nyingine Wananchi watarejea Tunisia ambako walikata tiketi ya kutinga makundi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Club Africain

Baada ya mchezo huo Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuikabili TP Mazembe katika mchezo utakaopigwa Februari 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Februari 26 Yanga itakuwa Mali kuwakabili Real Bamako kisha kurejea jijini Dar es salaam kwa mechi ya mkondo wa pili dhidi ya Real Bamako ambayo itapigwa Machi 07-08 2023

Machi 19 Yanga itawakaribisha US Monastir kutoka Tunisia katika mchezo wa mwisho wa nyumbani kabla ya kusafiri DR Congo kumenyana na TP Mazembe April 02 2023

Yanga inahitaji kukusanya alama zote tisa za nyumbani na kupata angalau sare mbili ugenini ili kujihakikishia tiketi ya kutinga robo fainali

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.