Klabu ya Yanga imerejesha Tsh Milion 112 kwa kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' baada ya kukataa maombi yake ya kuvunja Mkataba
Yanga imethibitisha kupokea barua ya Feisal na kiasi hicho cha fedha ikiwa na lengo la kuvunja Mkataba wake
Yanga imemtaka Feisal kifuata taratibu za kuvunja Mkataba kama ilivyoelekezwa katika Mkataba wenyenye pamoja na kanuni za FIFA na TFF
Aidha Yanga imethibitisha tayari ilishaanza mazungumzo na Feisal kwa ajili ya kuhuisha Mkataba huo lakini wameshangazwa na barua yake wakati mchakato huo ukiendelea. Mkataba wa Feisal na Yanga utamalizika May 2024