Type Here to Get Search Results !

Yanga, Feisal mbele ya Kamati ya Sheria leo

 

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo itajadili shauri la Yanga dhidi ya kiungo Feisal Salum 'Fei Toto'

Yanga ilimshitaki Feisal kwa Kamati hiyo 'kwa utoro' baada ya kuondoka kambini tangu Disemba 23 2022 kinyume na makubaliano ya mkataba

Kwa upande wa Feisal anadai ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake kwa mujibu wa makubaliano yake na Yanga

Feisal aliweka Tsh Milioni 112 kwenye akaunti ya Yanga ili kuvunja mkataba huo fedha ambazo hata hivyo Yanga walizirudisha na kusisitiza kuwa anapaswa kufuata taratibu ambazo zimeainishwa na TFF na FIFA

USIKOSE KUITAZAMA MECHI YA YANGA VS SINGIDA BIG STAR LIVE LEO BURE KUPITIA APP YETU BOFYA HAPA KUDOWNLOAD BURE

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.