Type Here to Get Search Results !

Simba kutimkia Dubai kesho - Mo awapa OFA hii

 

Rais wa heshima klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ametoa mwaliko kwa kikosi cha Simba kuweka kambi ya wiki moja Dubai kujiandaa na mechi za ligi kuu, ligi ya mabingwa na kombe la FA

Taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo, imebainisha kuwa msafara wa watu 38 utaondoka siku ya kesho Jumamosi kuelekea Dubai kwa ajili ya kambi ya siku saba

Katika sehemu ya maandalizi yake, Simba ikiwa Dubai inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki

Simba inatarajia kurejea nchini Januari 14 tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Januari 17

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.