Type Here to Get Search Results !

Breaking: Tff yatoa maamuzi haya, Feisal ni mchezaji halali wa Yanga

 

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeamua kuwa Feisal Salum bado ni mchezaji wa Yanga, kwa mujibu wa mkataba.

Uamuzi kamili kwa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa Jumatatu ya January 9, 2023.

Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko mbele ya Kamati hiyo ikipinga hatua ya mchezaji wao Feisal Salum Abdallah kuvunja mkataba kati yao bila kuwashirikisha.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo jana ambapo pande zote (Yanga na Feisal Salum) ziliwakilishwa na wanasheria wao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.