Type Here to Get Search Results !

TETESI ZA USAJILI : Kichuya kutimkia Yanga hizi hapa sajili zilizo kamilika mpaka sasa

 


DEAL DONE: AL ITIHAD YAKAMILISHA USAJILI WA DICKSON JOB

Kwa Mujibu wa Mtangazaji wa Ghana Micky Jr Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania Dickson Job amekamilisha Dili la kujiunga na Klabu ya Al ITIHAD 

"Done deal: Dickson Job (21) to Al Ittihad 🇪🇬 is confirmed to me some hours ago. 🇹🇿 Zoran Maki has landed his preferred defender in this transfer market. 🚨 More details soon.


YANGA WAIWINDA SAINI YA SHIZA KICHUYA

Taarifa zisizo Rasmi zinasema kwamba kocha wa Yanga Nasridine Nabi amewaambia viongozi wake kwamba anataka huduma shiza Ramadhani kichuya katika dirisha hili dogo la Usajili.

Taarifa zaidi inasema kwamba mazungumzo yameanza kufanyika kuhusu usajili wake wakati huo huo kuna baadhi ya wachezaji wataondolewa kwenye kikosi cha yanga akiwemo Crispin Ngushi

TETESI..

Club ya Simba imekamilisha Usajili wa beki wa Kagera sugar Abdala Mfuko

Simba wamefanya usajili wake kwa ajili kuendelea kuboresha timu kwenye michuano ya kimataifa na mashindano ya ndani

NKANE & NGUSHI WANAENDA IHEFU

Wachezaji wawili wa Yanga Crispin Ngushi na pamoja na Denis Nkane wanatakiwa na kikosi cha Ihefu.

Mpaka sasa mazungumzo yanaendelea vizuri katia viongozi wa Yanga na viongozi wa Ihefu kuwapeleka Wachezaji hao Kwa Mkopo.


TUYISENGE AMESAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC

Taarifa kutoka Kigali Rwanda zinasema kwamba tayari Club ya Simba imefikia makubaliano na mshambuliaji Jacques Tuyisenge .

Kumbuka msimu uliopita ilikuwa target yao kubwa ni kumpata Tuyisenge na Manzoki lakin ikashindikana.

Msimu huu katika dirisha hili dogo la Usajili wanataka kuhakikisha kwamba wanapata saini yake na taarifa kutoka Kigali zinasema kwamba tayari kila kitu kipo sawa.

Source Halisi Media


INONGA NI PASUA KICHWA MPAKA SASA SIMBA SC

Beki wa kimataifa wa Simba Henock Inonga amesema hataki kuongeza mkataba mpaka viongozi wa Simba wakubali kumpa mshahara mkubwa

Inasadikika kwamba mpaka sasa anataka mshahara wa Million 40 ili aweze kusalia kwenye kikosi cha Simba

Viongozi wa Simba wao wapo tayari kulipa kiasi cha shilingi million 30 kama atakuwa tayari kupokea kiasi hicho cha fedha.


YANGA WANAMTAKA EMANUEL KUTOKA RWANDA

Club ya Yanga ipo kwenye mazungumzo na beki wa pembeni raia wa Rwanda Imanishimwe Emanuel thamani yake inakadiriwa kufika mpaka Million 400.

Kwasasa anacheza kwenye club ya FAR Rabat ya nchini Morroco ,ana umri wa miaka 27 na yanga wapo tayari kumpa mkataba wa miaka miwili .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.