Mshambuliaji kinara wa mabao katika kikosi cha Simba Moses Phiri atakuwa nje ya uwanja kwa wiki moja akiuguza majeraha aliyopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar
Klabu ya Simba imetoa taarifa kuwa vipimo vya kitabibu vimebainisha kuwa Phiri alipata majeraha ambayo yatamlazimu kuwa nje kwa wiki moja hadi mbili
Hii ina maana Phiri atakosa mechi mbili za kuhitimisha mwaka 2022 dhidi ya KMC (Disemba 26) na Tanzania Prisons (Disemba 30)
Habari njema ni kuwa Phiri atapata muda zaidi wa kupona majeraha kwani mwanzoni mwa mwaka ligi itasimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi itakayoanza Januari 1, 2023