Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Kaze amesema mara nyingi Coastal Union ni timu inayowapa changamoto kila wanapokutana nayo. Lakini anaamini Yanga iko kwenye wakati mzuri zaidi kuwakabili wagosi hao wa kaya
"Tuna deni na mashabiki wetu kwenye mbio za ubingwa, naamini tuko vizuri kuwakabili Coastal Union, timu ambayo inatupa ushindani mkubwa kila tunapokutana," alisema Kaze
Kaze amesema pamoja na Coastal Union kutokuwa na matokeo mazuri katika msimu huu, timu hiyo ina wachezaji wengi wenye vipaji, hawapaswi kuwadharau
Akizungumzia utayari wa kikosi, Kaze amesema ukiondoa mlinda lango Aboutwalib Mshery ambaye ni majeruhi, winga Tuisila Kisinda alipata changamoto katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania na baada ya mazoezi ya mwisho leo, watafanya tathmini kuona kama ataweza kutumika hapo kesho
Mechi itakuwa LIVE kwenye app yetu kama bado hujaidownload ipakue Sasa