Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kaze amesema wanaelekea katika mchezo huo wakiwa kwenye wakati bora zaidi kwa mara ya kwanza katika msimu huu wakiwa na idadi ndogo ya majeruhi
"Tunakwenda kucheza na Polisi Tanzania tukiwa katika wakati bora kwa upande wa kikosi kwani wachezaji karibu wote wako tayari kutumika. Naamini tutakuwa na mchezo mzuri tukitafuta ushindi ili tuanze vizuri raundi ya pili ya ligi," alisema Kaze
Akizungumzia mchezo wenyewe, Kaze amesema wanafahamu wanakwenda kukutana na Polisi Tanzania ambayo imebadilika kiuchezaji baada ya mabadiliko ya benchi la ufundi lakini malengo ya Yanga ni kushinda kila mechi hivyo watakwenda kupambana ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi
Kaze amesema wachezaji wamepata muda mzuri wa maandalizi na kupumzika na hivyo wako tayari na watakaotumika siku ya kesho ni wale ambao wamefanya vizuri mazoezini
Amesema mlinda lango Aboutwalib Mshery ndiye mchezaji pekee ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi hapo kesho
NB: USIKOSE KUITAZAMA MECHI HII LIVE KWENYE APP YETU IPAKUE SASA HAPO JUU