Kikosi cha Yanga kilindoka mchana wa leo Alhamisi kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar
Yanga iliondoka na msafara wa wachezaji 19 baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza wakibaki jijini Dar es salaam kutokana na sababu mbalimbali
Wachezaji Khalidi Aucho na Joyce Lomalisa walipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc uliopigwa Disemba 25 na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2
Aucho anasumbuliwa na misuli ya paja wakati Lomalisa alipata majeraha ya nyonga
Aidha Yanga imethibitisha kuwa winga Bernard Morrison amepewa ruhusa ya kusafiri kwao nchini Ghana kushughulikia matatizo ya kifamilia
Djuma Shabani nae atakosekana akisumbuliwa na malaria wakati Denis Nkane anaendelea na matibabu ya majeraha ambayo yatamuweka nje kwa wiki sita
Wachezaji waliosafiri kwenda Morogoro;
Djigui Diarra, Erick Johora, Shomari Kibwana, Bakari Mwamnyeto, Yanick Bangala, Dickson Job na Ibrahim Bacca
Wengine ni Gael Bigirimana, Zawadi Mauya, Salum Abubakari, Jesus Moloko, Farid Mussa, Dickson Ambundo, David Bryson, Tuisila Kisinda na Yusuph Athumani
Pia wamo Clement Mzize, Stephane Aziz Ki na Fiston Mayele